Mkurugenzi wa Tanzania One Thetre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa
Mbinga Magharibi, John Komba akizunguma na waandishi wa habari nyumbani
kwake, Mbezi Tangi Bovu, Kawe, Dar es Salaam, leo wakati akizungumzia
hali ya afya yake baada ya kurejea nchini akitoka nchini India alikokwenda
kufanyiwa upasuaji. Kushoto ni Mkewe, Salome Andrew Komba.
**********************************
NA BASHIR
NKOROMO
MKURUGENZI
wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi,
John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa
nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.
Akizungumza
na waandishi wa habari, jana Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi kwa Komba,
mjini Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini, Juzi, baada ya
kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India
tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Alisema,
aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo
ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John
Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu
ya mgomo wa madaktari.
"Siku
napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo
wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake akanisaidia
haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje", alisema
Komba.
Alisema,
uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu
wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati
wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo
90 au 100 tu.
"Amesema,
baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo
ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika
kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama
alivyoelekezwa na madaktari.
Akizungumzia
upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila
matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa
wa futi moja.
Alisema,
hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa
sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika
kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku
tano.
"Sasa
nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito
uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa",
alisema Komba.
Komba
alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua
kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.
"Jamani
ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo
kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua
figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa
nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika
ninachoumwa", alisema Komba.
0 comments:
Post a Comment