Friday, July 13, 2012

........BADRA KUJA KUWASHIKA WANA HIP HOP.......

WAKATI wengine wakiukimbia muziki wa Hip Hop msanii anayetesa ndani ya bongo muvi, Badra, amesema kuwa anaamini muziki wa huo utamlipa kwani ana kipaji na uwezo mkubwa wa kufanya michano kuliko hata wale walio kwenye fani hiyo kwa muda mrefu.

Msanii huyo akiongea na DarTalk alidai kuwa tangu awali alikuwa akipenda sana muziki huo lakini alikuja kuachana nao na kujikita kwenye tasnia ya filamu lakini kwa sasa anakuja na nguvu zote huku akiaamini ushirikiano mzuri na wasanii waliopo katika tasnia hiyo ndiyo utakaompeleka mbali zaidi.

Alisema kuwa hataacha kuwa karibu na wasanii wengine wakubwa wa tasnia hiyo ambao tayari wanajulikana kwani anaamini anataweza kujifunza mambo mengi kuhusu muziki ya mziki kupitia wao.

‘‘Nafanya muziki wa hip hop si kwa kuiga bali nina uwezo huo hivyo naomba mashabiki wangu ambao wamenizoea kuniona kwenye filamu sasa wajue kuwa hata kwenye muziki pia naweza vilevile, alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms