Wednesday, February 22, 2012

.......KANUMBA ATOA UJUMBE MZITO.......

MUIGIZAJI nyota na mtayarishaji mahiri wa filamu Swahiliwood, Steven Kanumba amewahimiza wasanii kujiunga na vyuo vya filamu vinavyoanzishwa nchini badala ya kukimbilia kuigiza moja kwa moja.

Anasema watayarishaji wa filamu wamekuwa wakilazimika kuwatumia wasanii wasio na sifa katika fani hiyo ya uigizaji na akadai kuwa anakerwa na utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wasanii.

Ni vema wakajiunga na vyuo vinavyofundisha fani ya uigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza. Sanaa bila elimu ni sanaa dumavu.

Nimebahatika kusafiri katika nchi kadhaa, naona umuhimu wa kujiendeleza hata kama una kipaji, mara nyingi napata wakati mgumu kila asubuhi ninapoamka na kuwakuta vijana wakinisubiri nyumbani kwangu huku kila mtu akisisitiza kuwa yeye ana kipaji na anahitaji kufanya kazi na mimi, lakini ukimpa nafasi hali inakuwa tofauti na maongezi yake, anasema Kanumba.

Anasema kuwa hali ya sasa ya tasnia ya filamu inakabiliwa na changamoto nyingi hasa baada ya maigizo kupunguza msisimko wake katika televisheni, jambo ambalo watayarishaji wanajikuta wakiwatumia wasanii ambao hawajawahi kupitia katika vikundi vya maigizo ambao wanaamini kuwa wanafuatwa kwa sababu ya urembo wao au umaarufu, hivyo kukosa uchungu na sanaa.

Hawa wasanii ambao hawajapitia katika makundi ya maigizo ni shida, ndiyo maana tunalalamikiwa sana kuwa wasanii tumekosa maadili, lakini si wote.

Hawa wenzetu wameingia kirahisi sana, lakini nakumbuka nilikaa katika kundi la Kaole zaidi ya mwaka kwa kufanya mazoezi bila kuonekana katika Televisheni, ukimwona msanii anaigiza unatamani, unajitahidi kufanya mazoezi kwa bidii, nawaasa kuwa wavumilivu na nidhamu mtapata matunda kama sisi, anasema Kanumba

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms