Monday, October 22, 2012

.....TRA BANKS AKARIBISHA KIDUME.....

TAKRIBANI miaka kumi sasa mashindano ya America's Next Top Model yamekuwa yakishirikisha wanawake pekee, lakini kuanzia mwaka ujao yatajumuisha wanaume pia.

Mtayarishaji wa mashindano hayo, Tyra Banks ametangaza kuwa kuanzia msimu ujao mashindano hayo yatatafuta vijana wa kike na wa kiume tofauti na miaka ya nyuma.

Alisema wote wataishi katika nyumba na watawania taji moja tu. Mshindi wa mwakani wa ANTM anaweza kuwa mwanamke au mwanaume.

Mashindano hayo ambayo hurushwa moja kwa moja katika televisheni yalianza mwaka 2003. Huwa yanatafuta wasichana katika vyuo wenye ndoto za kuwa wanamitindo na kuwashindanisha kisha kuwaendeleza.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms