Tuesday, October 9, 2012

....SKENDO ZA WASANII ZINACHAFUA TASNIA YA FILAMU......


MSANII nguli anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo Monalisa, amefunguka na kudai kuwa huwa anatokwa na machozi pale anapoona wasanii wengine wa tasnia hiyo wanafanya mambo ambayo yanaipelekea fani hiyo kuonekana ya kihuni.

Msanii huyo unaweza kusema ni moja kati ya nyota wanaofanya filamu za viwango vya kimataifa, na ndiyo maana ameweza kufika mbali ikiwemo kuingizwa kwenye tuzo kubwa kubwa za kimataifa.

Monalisa alisema kuwa mara nyingi huwa anashindwa kuelewa ni kitu gani kinachosababisha msanii kufanya mambo ya ajabu badala ya kutulia na kubuni vitu vya kufanya kwa faida ya taifa na tasnia kwa ujumla, wasanii wa nje wanapata umaarufu kupitia kazi zao ambazo zinadumu sokoni kwa muda mrefu kutokana na umakini wao.

“Kila msanii anajua anafanya nini kwenye tasnia hii lakini wote kwa pamoja lazima tujue kwamba hakuna filamu ambayo tunaweza kusema imetikisa dunia kutoka Tanzania, hivyo tunajukumu kubwa la kubuni vitu ili nchi yetu ifike mbali kupitia filamu, lakini wasanii wetu hawafikilia kitu kama hicho,” alidai.

Aliongeza kuwa kuna mitazamo feki ndani ya tasnia hiyo kuwa msanii hawezi kuwa maarufu bila skendo ambapo kwa upande wake anaamini hiyo haina maana kwa kikubwa kinachoweza kumtangaza msanii ni kufanya kwa nzuri.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms