Monday, October 15, 2012

.......SIJALI UPWEKE......NIKO SAWA......

NINAFURAHIA maisha haya bila kuwa na mpenzi ingawa si vema kwa mwanamke wa umri wangu kuwa peke yake, lakini ninamsubiri mwanamume niliyepangiwa na Mungu."

Hayo ni maneno ya Vivica Fox ambaye sasa ameamua kukaa pembeni na mapenzi ingawa anakiri hamaanishi kuwa hataingia mapenzini tena.

"Ninajua mapenzi yana umuhimu wake katika maisha, hasa kwa mtu wa umri mkubwa, lakini nimepumzika kwa sasa," alisema.
Hata hivyo, amekanusha vikali kuwa amekuwa akiingia katika mitandao ya kutafuta wapenzi maarufu kama 'dating sites' kwa ajili ya kutafuta mwenza.

Alisema huo ni upuuzi ambao unaweza kufanywa na wahuni tu.
Siwezi kufanya upuuzi wa kuingia mtandaoni kutafuta mwenza, kwani nina kasoro gani hadi nikose katika maisha ya kawaida?

Ninataka kukutana na mwanaume ana kwa ana, tena kabla ya kuanza mapenzi lazima tutoke 'out' mara nyingi," alisema Vivica.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms