Friday, October 12, 2012

........‘RAY’ KUACHIA FILAMU MPYA ‘SISTER MARY’, IRENE UWOYA, ‘JOHARI’ NDANI…....

MSANII nguli wa filamu Tanzania, Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa hivi karibuni anatarajia kuachia filamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Sister Mary’, iliyofanyika chini ya RJ Company ambayo itakuwa na nyota wengine kama Irene Uwoya, Johari na wengine kibao ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu nchini. Ndani ya mzigo huo Uwoya amecheza kama Sister Mary na Ray amecheza kama Father Criss.

Ray alizungumza na mtandao wa huu na kusema kuwa zipo filamu nyingine ambazo zinakuja lakini hiyo imeshakamilika na mashabiki wake wataanza kuitazama pia imetengezwa katika kiwango cha hali ya juu.

“Hiyo ndiyo filamu ambayo inakuja kwa sasa na nipo na wasanii wengi wazuri ambao wanafanya vizuri na kila msanii amecheza vizuri kulikana na nafasi yake, hata hivyo nawaomba mashabiki wangu wanipe sapoti yao kwani bila wao mimi siwezi kusimama na kufanya filamu,” alisema,

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms