Monday, October 22, 2012

.......NINA KIFAA KIPYA.....

MWANAMUZIKI, Cheryl Cole anasema mpenzi wake mpya, Tre Holloway ameweza kumsahaulisha machungu aliyoyapata miaka miwili iliyopita.

Cheryl ambaye ni mke wa zamani wa mchezaji wa Chelsea, Ashley Cole alisema kwa zaidi ya mwaka mmoja alikaa bila mpenzi ili aweze kusahau adha aliyoipta katika ndoa.

"Hatimaye sasa ninahisi kuwa na furaha tena katika maisha yangu, Tre ni mwanamume mtanashati ambaye ameweza kunisahaulisha machungu yote niliyoyapata nyuma, " anasema Cheryl.

Cheryl anasema alikosa mwelekeo baada ya kuachana na mumewe mwaka 2010. Aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Marekani, Will.i.am na mcheza shoo, Derek Hough.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms