Thursday, October 18, 2012

.....NAMZIMIA SANA NEY JAMANI.....

MWIGIZAJI wa kike katika ya tasnia Swahiliwood Asfa Omary Neema 20% ameshindwa kuficha hisia zake pale alipodai kuwa pamoja na umri wake mdogo anamzimia sana msanii wa Bongo fleva, Ney wa Mitego.

"Si siri nampenda sana Ney wa Mitego na natamani awe mume wangu wa ndoa hata kesho kama akikubali, kama ingekuwa wasichana tunaruhusiwa kuwatongoza wanaume na kuolewa nao basi mimi ningekuwa wa kwanza kwa Ney, ana mvuto na shababi, analonga Neema 20%.

Neema msanii aliyevuma na kuibuka kupitia filamu ya 'Furaha Iko Wapi' iliyotungwa na msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamis Kinzasa "20 Percent" amedai kuwa anampenda mwanamume anayejiamini na kuwa mtanashati muonekano anaouona kwa msanii Ney na si mtu mwingine, na hatafanya kila juhudi ili aweze kuishi na msanii huyo

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms