Friday, October 5, 2012

........MSIMSOGELEE DIANA HATAKI MWANAUME.......

DIANA Exavery amesema anahitaji kuwa huru zaidi kwa kutokuwa na uhusiano na mwanaume yeyote akiamini uhusiano unaweza pia kuathiri kazi zake.
"Katika maisha yangu nahitaji sana kuwa huru, ninajua uhuru wa mwanamke unapatikana pale anapokuwa hana mahusiano na mwanaume," alisema.
"Unajua ninapokuwa huru sipati mtu wa kunisumbua na kunizuia kazi zangu za sanaa kwa ujumla."
Msanii huyu alianza kung'ara katika filamu ya Mtunis iliyojulikana kwa jina la 'Best Wife', baadaye alishiriki katika filamu ya 'Mrembo Kikojozi', pia filamu ya 'Yatima Asiyestahili' na hivi karibuni ameigiza katika filamu ya 'Binti Yangu' akiwa mhusika mkuu.
Kuthibitisha msimamo wake, Diana, anasema ndiyo maana kwa sasa hana rafiki wa kiume, mchumba wala mume.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms