Wednesday, October 17, 2012

.....MIMI NI TAJIRI WA MAVAZI AISEEEE....


MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Dansi Bongo Patcho Mwamba Tajiri anasema kuwa mavazi anayovaa pamoja na kuwaazima wasanii wengine anaokutana nao wakati wa kurekodi filamu ni mali yake na hajawahi kuazima.

Mavazi ninayaotumia kwa kila filamu ninayoigiza ni ya kwangu mwenyewe hakuna kampuni ya mavazi wala duka linalonivalisha katika filamu ninazoigiza, sijawahi kurudia nguo katika filamu ninazoigiza kwa sababu nina nguo nyingi za kutosha za kila aina ikiwa pamoja na viatu saa za kutosha Cheni na vitu vingine,anasema Patcho.

Msanii huyo pamoja na kuigiza filamu zaidi ya 50 hadi sasa ndiye anayetegemewa na baadhi ya waigizaji katika kuwaazima nguo kwa ajili ya kuigizia, huku bado akiendelea kung
ara kwa kujikwamua katika kadhia ya kuazima mavazi au kukodi jambo ambalo uwatesa wasanii wengi kwani kulingana na udogo wa bajeti za filamu hizo inawawia vigumu kumudu kununua nguo za kuigizia kwa kila filamu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms