Monday, October 15, 2012

..........BEYONCE AMPIGA CHINI CLINT EASTWOOD.....


STAA wa 'I was Here', Beyonce Knowles, amesema ameshindwa kufanya kazi na Clint Eastwood kutokana na kubanwa na majukumu mengine.

Clint alitangaza mapema mwaka huu kuwa atafanya kazi na Beyonce katika filamu yake mpya, 'A Star Is Born' lakini mara kwa mara waliahirisha kazi hiyo kwa kuwa Beyonce hakuwa na nafasi.

Hata hivyo Beyonce aliamua kumweka wazi kuwa Clint ni bora atafute mtu mwingine kwa kuwa sasa ana majukumu mengi ikiwamo kumpigia debe Rais Barack Obama katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani.

Nilikuwa na hamu sana ya kufanya kazi na Clint, kwa miezi mingi sasa tumejaribu kuangalia uwezekano huo lakini imeshindikana, natumaini katika siku zijazo tutaweza kufanya kazi," alisema Beyonce.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms