Saturday, August 11, 2012

.........‘SINTAH’ KUPOTEZA SHAVU LA ‘UNAMID-UNITED NATIONS MISSION IN DARFUR’ ???.......


BAADA ya kuingia kwenye skendo ya kutoa picha za binti mwenzake mitandaoni msanii Sintah, huwenda akapoteza nafasi yake aliyopewa hivi karibuni kuwa Balozi wa UNAMID – United Nations Mission In Darfur.

Msanii huyo alipata kazi hiyo baada ya kuonekana ni mmoja kati ya wasanii wanajituma na kutafuta maendeleo, pia hayupo kwenye maskendo ya kumchafulia jina, lakini baada ya hii ya kutoa picha za utupu za Agnes Gerald kwenye mitandao inaweza kumfanya akatolewa kwenye nafasi yake.

Baadhi ya wasanii ambao wameshtushwa na ishu hiyo, bila kutaja majina yao, walidai kuwa nafasi aliyokuwa nayo Sintah ni kubwa na mambo anayoyafanya yanatia aibu kitu ambacho kitamfanya apoteze heshima yake.

Kwa upande wake Ray ambaye ndiye rafiki yake wa karibu kwa sasa, alidai kuwa haoni kama Sintah anaweza kupoteza nafasi hiyo, uwezo wake ni mkubwa na ishu hiyo ilitokea kwake na Agnes si ya kuweza kuchukuliwa kama sababu.

Kwa upande wake muhuka mkuu wa ishu hii Sintah, alidai kuwa hafikilii kama kuna uwezekano wa kupoteza nafasi hiyo kwani tatizo si lake ni la mtu mwingine zaidi ya yote yenye amewekwa kama kufuta ushahidi wa aliyeonekana naye humo katika uchafu wa Agnes.

“Uchafu uliofanywa na mtu mwingine hauwezi kunifanya mimi nishindwe kuishi mjini vizuri naamini alichokifanya hadi alikuwa anataka kunifanya mimi niwepo kwenye ishu yake, pia suala alilosema kuwa anataka kuweka picha zangu chafu mitandaoni najua hawezi,” alidai Sintah.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms