Wednesday, July 4, 2012

.........YUKUTI KANIDHULUMU- NICE.......

MWANDISHI wa muswada wa Swahiliwood, Ali Yakuti ameshutumiwa kwa kumdhulumu mwigizaji wa filamu za Bongo, Godliver Godian Nice malipo yatokanayo na ushiriki wa filamu ya 'Who Is The Looser'.

Filamu hiyo iliandaliwa na mwandishi huyo na kwenda kurekodiwa huko Kibaha. Msanii huyo amedai: "Naamini karibu washiriki wote wa filamu ya Yakuti wamelipwa, lakini kwangu imekuwa shida, ukimpigia simu hapokei, lakini jambo la pili baya zaidi linalonifanya roho iume zaidi ni jinsi nilivyojitoa katika filamu hiyo.

"Yaani nilizimika hata kufanya kazi nyingine tofauti na ile ya kuigiza, najiuliza kwanini hataki kunilipa fedha ambayo ni jasho langu?"

Nice amesema kuwa wakati filamu hiyo ikirekodiwa hakukuwa na mtu wa mapambo (Make Up) kazi ambayo aliifanya kwa ajili ya kuifanya filamu hiyo iwe bora.

Anasema kuna wakati Yakuti alimpigia simu akimtaka kurudia vipande vya filamu hiyo, jambo ambalo hata yeye lilimshangaza.

"Nikamkumbushia fedha zangu, akasema atanipa na pia tukapanga siku ya kurudia vipande hivyo, lakini siku ilipofika Yakuti hakupokea simu yangu," alisema.

Unajua mimi niliacha kazi kwa ajili ya kurekodi kazi yake kwa sababu pamoja na kusomea fani nyingine lakini napenda sana kuigiza, nimekaa Kibaha zaidi ya wiki halafu mtu bila huruma anakudhulumu jasho lako hakupi hata senti tano! Inauma sana,anasisitiza Nice.

Mwanaspoti ilimtafuta Ali Yakuti kwa njia ya simu lakini simu yake iliita tu na baada ya muda haikupatikana tena.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms