Wednesday, July 25, 2012

.....WASANII WAKIKE NIGERI WENYE MAUMBO MAKUBWA NI DILI.......

KAMA ilivyo sehemu nyingi duniani, hata Nigeria sura za wasanii wa kike wenye maumbo makubwa ndizo hutawala kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku na majarida ya burudani.

Wasanii hao wanageuka gumzo la majiji kama Lagos na Abuja haswa inapotokea hafla kubwa hususani zile za usiku.

Hii ni kutokana na maumbo yao makubwa ya mwili na jinsi wanavyopenda kuvaa nguo ambazo huacha wazi sehemu kubwa za miili yao haswa matiti.

Mastaa hao wengi wao wamekuwa wakikiri hadharani kwamba si kitu cha ajabu kufanya hivyo kwani kila mmoja ana utaratibu wake wa kuvaa hasa kwenye matukio maalum ya usiku.

Hivyo kwao kama kuna mapaparazi wanawafuatilia ni juu yao. Watajiju. Wengi wa wasanii hao huvaa saizi 12 au zaidi.

Wakikupitia karibu lazima usisimke na ugeuke nyuma kuwaangalia hata mara tano.

Ifeoma Okeke
Ana mvuto halafu ni mpana, anajua kutinga staili za aina yake ambazo akipita lazima ugeuze shingo. Licha ya unene wake, lakini anaamini kwamba hana mpinzani kwenye suala la mvuto.

Alitamba na filamu ya Evil Genius na kila siku anazidi kupanuka tu. Amesema kwamba hajisikii vibaya kwa jinsi alivyo na wala haoni cha ajabu.

Marafiki zake wa karibu wamedokeza kwamba anakaribia kufikisha uzito wa kilo 200 na wamekuwa wakimshauri kujiangalia mara mbili.

Chioma Toplis
Mwenyewe amejiangalia na kukiri kwamba katika miezi ya karibuni uzito umekuwa ukipanda kwa kasi mpaka anashangaa.

Amesisitiza kwamba tayari ameanza mazoezi makali kujiweka fiti ingawa bado hajaona dalili ya kupungua.

Habari za uhakika zinadai kwamba amekuwa hapendi mambo ya kuchanganya akili yake katika miezi ya hivi karibuni kwa vile anaogopa kufa kwa kisukari na presha.

Wengine wanajiuliza, je? Kwa Manyama uzembe aliyoendekeza ataendelea kuwa na mvuto siku zijazo?

Eniola Badmus
Ana bonge la kitambi siku hizi na wala hajawahi kusikika akilalamika. Msanii huyo maarufu kwa jina la Gbogbo Big Girl, ni binti anayependa kujipodoa ingawa hakuna uhakika kama anajua madhara yake.

Uchunguzi unaonyesha kwamba mwili wake mkubwa ndiyo umemfanya akawa maarufu zaidi kuliko kazi anazofanya.

Adaora Ukoh
Marafiki zake wamesikika wakimuonya mara kadhaa, lakini ni kama vile anaona yuko sawa.

Miezi michache iliyopita alizindua gauni kubwa alilolipa jina la Adaora akiwa anamaanisha kwamba ni nguo maalum kwa ajili ya wasichana mabonge kama yeye.

Anaamini kila mwanamke ni mrembo na uzuri uko ndani na si ukubwa wa mwili japokuwa ameanza mazoezi ya gym.

Foluka Daramola
Foluke Daramola anaijua kazi yake, acha apewe sifa. Lakini mashabiki wake wamekuwa wakiguna kila wanapomuona kutokana na unene wake mkubwa. "Unene au mwili wa mtu ni suala binafsi la maisha ya msichana hakuna wa kumuamulia, najua ninachopaswa kufanya," ndivyo anavyosema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms