Monday, July 30, 2012

......TUHAKIKISHE TUNANUFAIKA NA KAZI ZETU......

WASANII wa fani ya vichekesho wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanapata maslahi kupitia kazi zao na isiwe wanafanya kazi ya kutafuta sifa tu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Rashid Costa 'Maringo 7' msanii anayeunda Kundi la Mizengwe, anasema suala la kuendekeza sifa tu limesababisha kudharaulika kwa fani hiyo.

"Tusipokuwa makini tunajiua wenyewe, wengi wetu huwa wanakubali kuuza kazi zao kwa bei ya hasara hii ni hatari. Soko la Komedi linakuwa baya kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele," alisema.

Msanii huyo anayetamba na lafudhi yake ya Kikongo, aliongeza kuwa inawezekena kabisa kwa fani hiyo kufanya vizuri sokoni na kuwafaidisha wahusika kama wasanii wenyewe watajijali na kukikuwapo usimamizi mzuri wa usambazaji wa kazi.

Juhudi zianze kwetu wasanii kabla ya kuwashirikisha wadau wengine, tusifanye kazi ya kujifurahisha tu bali tuhakikishe inatusaidia kuweza kuendesha maisha, hilo linawezekana endapo tutashirikiana pamoja," alisisitiza.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms