Saturday, July 28, 2012

........RAY AWAPA KWELI MA-MISS WANAOKIMBILIA KWENYE TASNIA YA UIGIZAJI.......

IDADI kubwa ya warembo wanaofanya filamu ndani ya bongo ni wale waliopita katika mashindano ya ulimbwende iwe wa vitongoji au Taifa, ambapo msanii nguli ndani ya tasnia hiyo Vicent Kigosi ‘Ray’, ametoa somo kwa warembo wengine kuwa wasifikilie tasnia hiyo ni kimbilio lao baada ya kutoka kwenye mashindano yao.

Ray alikaririwa na mwandishi wa DarTalk, akidai kuwa anaamini Tanzania inaweza kupata wanamitindo wazuri lakini anashindwa kuelewa ni kwanini wengi wanakimbilia kufanya filamu baada ya kutoka kwenye mashindano ya U-miss.

Alidai kuwa inawezekana tasnia hiyo ya filamu haina thamani kwani kila mrembo aliyepitia mashindano ya U-miss, baada ya kutoka huko basi anaingia kwenye filamu na kuachana na fani yake ambayo wenda ingeweza kuwa ndio fani yake.

Aliongeza kuwa kila mrembo anayeingia kwenye filamu anadai kuwa fani hiyo ya uigizaji ipo ndani ya damu, hapo ndipo anaposhindwa
kuelewa kwamba kama filamu ni fani inakuwaje aliingia kwenye kwenye ulimbwende on the first place.

“Nawaomba tu warembo wanaotokea kwenye fani hiyo, kama kweli wanahitaji kuliwakilisha vyema taifa letu basi wakaze buti kwenye fani hiyo kwani ni kitu cha aibu sana wanaposhindwa huko na kuja huku kwenye filamu, wanakosa muelekeo”. alisema

Ishu hiyo ndiyo inayofanya hadi tasnia ya filamu Tanzania ishindwe kupiga hatua kwani matatizo kibao yanayotokea ndani ya tasnia hiyo yanasababishwa na wasanii waliotokea kwenye U-miss.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms