Friday, July 13, 2012

......BIFU LA WANAGHANA NA WANANIGERIA NI BICHI.....

MAMLAKA za Ghana zimeanza msako maalumu wa kuwaondosha nchini mwao wafanyabiashara wa kigeni wanaomiliki ardhi kinyume cha taratibu au kufanya biashara bila kibali.

Zoezi hilo ambalo limepamba moto limeanza kuathiri wageni wengi, asilimia kubwa wakiwa ni jirani zao Nigeria ambao walikuwa wakiwekeza kwenye biashara mbalimbali.

Raia wa Nigeria walioko Ghana wameandamana kwa madai kuwa wanaonewa, lakini nyumbani Nigeria nako wengine wametengeneza mabango yanayowataka Waghana nao watimkie kwao wawaachie nchi yao.

Imekuwa kama uhasama baina ya nchi hizo zilizo na mahusiano ya kibiashara kwa muda mrefu. Hilo limekaa kisiasa zaidi, huku kwenye filamu na kwenyewe bodi na wasanii wa nchi hizo mbili wana bifu la aina yake ambalo kila leo limezidi kuchukua sura mpya.

Nollywood na Ghollywood hazina ushirikiano wa dhati huku kila upande ukijiona uko juu ya mwingine.

Nollywood ndiyo imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuteka sehemu kubwa ya soko la filamu za Afrika huku wenyewe wakijinadi kwamba ndiyo wa pili kwa mauzo duniani, yaani baada ya Hollywood ya Marekani.

Baadhi wanadai kwamba Waghana ndiyo walioanza kuingia kwenye filamu za Nollywood tangu kuasisiwa kwake na wamejifunza mambo mengi zaidi kutoka kwa wenyeji.

Lakini wengine wanaamini kuwa Waghana wanajua sana na ndiyo wamechangia kuwakuza Wanigeria kiteknolojia kwenye mambo ya filamu.

Lakini upande mwingine unasema kuwa Ghollywood ilianza baada ya Nollywood ndiyo maana wanatofautiana kiubora na umaarufu.
Pia wasanii wake wengi wanazamia Nigeria ambako wanaona kunalipa zaidi na rahisi kujulikana.

Wanigeria wanadai kuwa Ghollywood iko chini yao ndiyo maana imekuwa ikitumia wasanii wengi wa Nollywood kujipandisha.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms