Tuesday, July 17, 2012

......“BAJETI YA FILAMU ZANGU HUWA HAIPUNGUI SH. MILIONI 25″ – JACKLINE WOLPER…....

BAJETI za wasanii wengi wa kibongo wanapotengeza filamu zao ni chini ya milioni 7, lakini msanii wa filamu bongo Jackline Wolper, inadaiwa kuwa ni nyota pekee anayetengeneza filamu kwa gharama kubwa kuliko msanii yeyote Tanzania.

Mmoja wa rafiki wa karibu na msanii huyo ambaye huwa karibu karibu upangaji wa bajeti katika filamu zake, aliyekataa kutajwa kwa jina lake, alidai kuwa msanii huyo hutumia sh mil 25-30 katika filamu moja kiasi ambacho hakuna msanii yeyote anawefikia.

Alidai kuwa wasanii wengi wa kibongo hutengeneza filamu kwa mil 5-7, ingawa kiasi hicho ni kikubwa, kwani hata wale wasanii wanaoshiriki katika filamu hizo, wanalipwa kaisi kidogo cha pesa.

“Wolper amekuwa msanii namba moja katika kutengeneza filamu za gharama, na pesa hizo zinatumia katika malipo ya wasanii, hivyo unazani kama angedkuwa anatumia mil 7, katika kutengeneza filamu hata hao wasanii waoshiriki watalipwa kiasi gani,” alihoji.

Aliongeza kuwa wapo baadhi ya waandaaji wa filamu wengine ambao huwalipa wasanii sh 50,000 na kiwango cha juu sana ni sh laki moja ‘100,000′ lakini kwa upande wa Wolper huwalipa kiasi kikubwa cha pesa wale wanaoshiriki katika filamu zake.

Katika kuweka usawa wa ishu hiyo alitafutwa Wolper ili kuweka wazi kauli hizo za rafiki yake kama ni kweli hutumia kiasi hicho cha pesa, na baada ya kupatika alijibu kuwa filamu zake hutumia kiasi kikubwa cha pesa na hii inatokana na kujua umuhimu wa kazi hiyo pamoja na wale wasanii anaowatumia kwani wanakuwa wameacha kazi zao nyingine.

“Mimi siwezi kumtumia msanii na kumlipa hela ya chakula eti nimemlipa, najua hii ni kazi hivyo kila mtu anatakiwa kulipwa kiasi ambacho najua kitakuwa fair, huwa tunalipa kuligana na nafasi ya mshiriki katika filamu,”. alisema

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms