Tuesday, June 26, 2012

....WIMBO HUU " NAKUNGOJA" UMENIGHARIMU 1.5 MILIONI.....


WANA Misosi ambaye amewahi kufanya kazi na Redsun wa Kenya pamoja na Jose Chameleone wa Uganda, amekamilisha wimbo mpya wa Nakungoja akisema umemgharimu Sh1.5 milioni.

"Kulikuwa na changamoto nyingi ambazo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nimeweza kuzikabili. Nimerekodi na video yake kabisa na kazi nimeshaisambaza katika vituo mbalimbali vya runinga," alisema.

Bwana misosi amesema kuwa katika wimbo huo amemshirikisha msanii chipukizi anayeitwa Migigi ambaye amefanya vizuri katika mashairi yake.

Alisema wimbo huo wenye mahadhi ya Raggae umetengenezwa katika studio ya Combination Sound chini ya Man Water wakati video imetengezwa na Bongo Land Picture.

Mkali huyo mwenye taaluma ya mambo ya umeme alianza kutambulika katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya baada ya kuachia kibao cha 'Nitoke Vipi'.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms