Wednesday, June 20, 2012

....UWOYA ATOA SOMO KWA WASANII WENZAKE....


MWIGIZAJI nyota wa filamu za Swahiliwood, Irene Uwoya, anaamini kuwa uwepo wa tuzo katika tasnia ya filamu unaweza kuleta chachu kwa waigizaji na watayarishaji kwa ujumla.

Uwepo wa tuzo katika tasnia ya filamu utaongeza ufanisi na ubora wa kazi zetu za filamu, tuzo zitatufanya tufanye kazi nzuri zaidi ili kuingia katika ushindani, natoa wito kwa waigizaji wenzangu kufanya kazi kwa umakini ili kuleta msisimko na ushindani zaidi kwa waigizaji, watayarishaji na wadau wote katika tasnia ya filamu," alisema Uwoya.

Tuzo za filamu kwa mara ya kwanza zilitolewa Tanzania mwaka 2005/2006 kisha ukapita mwaka mmoja ndipo zikaja za Vinara mwaka 2010/2011 zilizotolewa na mtandao mahiri wa habari za filamu Swahiliwood wa filamucentral. Baada ya hapo hakuna nyingine.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms