Friday, June 29, 2012

....TOFAUTI YA FILAMU ZA NOLLYWOOD NA HOLLYWOOD BADO KUBWA........


LICHA ya kwamba filamu za Nigeria maarufu kwa jina la Nollywood ndizo zinazoongozwa kwa mauzo barani Afrika, bado kuna tofauti kubwa kati ya filamu hizo na zile za Marekani Hollywood.

Ukifuatilia filamu nyingi za Nollywood, utagundua udhaifu ufuatao ambao huwezi kuukuta katika kazi za Hollywood.

Jina linakutambulisha maana ya stori nzima, wala huhangaiki kuumiza kichwa na Mwanamke atakwenda kulala usiku wakati uso wake umejaa vipodozi kama kwamba ndiyo anajiandaa kwa mtoko.

Mtu anaonyeshwa kama ana miaka 25 lakini bado atakuwa amevaa mavazi aliyokuwa ametinga siku za nyuma wakati anakua.

Kama filamu inazungumzia matukio ya mwaka 1980 mpaka 1990, ndani yake utaona mabango ya kampuni za simu za MTN, ETISALAT na GLO ambazo zimeanza miaka ya 2000.

Mashairi ya nyimbo zinazotumika kwenye filamu yanazungumzia kila kitu kilichopo kwenye filamu husika na wimbo huo utausikika kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa filamu bila kujali ni sehemu ya mahaba, ngumi au kichekesho.

Mwigizaji anatumia dakika 15 akitishia kuua mtu, mwingine atatumia dakika tano kuishangaa silaha yake(huku mtuhumiwa au anayetishiwa akishangaa bila kukimbia), halafu watatumia tena dakika nyingine kutishiana.

"Nitakuua leo" baada ya 'kumshuti' yule aliyeumizwa akiwa anagalagala chini anasema "Nimekufaaa.., umeniuaaa.., nakufaaa..." halafu anakufa.

Matangazo ya filamu mpya zijazo yanatawala karibu nusu saa mwanzo wa filamu. Gari likiwa na spidi kali litamgonga mtu halafu mtu huyohuyo ataendelea kulala hapohapo chini kana kwamba hajaumia sana.

Usipopunguza sauti huwezi kusikia waigizaji wanachozunguza, sauti ya wimbo iko juu kuliko wanachosema wasanii.

Kila ukimwona binti anayetoka kijijini lazima aongee lafudhi ya kikwao.
Lazima mwisho wa filamu ukutane na neno hili "To God Be The Glory Watch Out For Part 2".

Halafu karibu filamu zote lazima ziishie kanisani kwa mchungaji na wafuasi wake na aliyekosa anaungamishwa na kumrudia Mungu filamu inaisha.

Hata mzimu kwenye filamu lazima utatazama pande zote za barabara kabla ya kuvuka, mwanamke anavaa nguo za kuendea klabu za usiku kila siku hata kama anapika jikoni au anahudumia watu ghalani.

Matangazo yote ya filamu yanaisha na neno "Go and grab ur copy now" na msanii anaonekana akitoka nyumbani na shati jekundu kwenye gari anaonekana na shati la rangu ya bluu na anapofika anakokwenda ana shati jekundu tena.

Kila mgonjwa atakayefia hospitali lazima ajigaragaze kitandani kabla ya kukata roho. Jim Iyke anaingia kwenye klabu ya usiku na miwani ya jua huku filamu ikionyesha watu wanacheza kwa zaidi ya dakika 15 ndani ya klabu ya usiku bila tukio lolote wala kuzungumza.

Aki na Paw Paw lazima waigize filamu moja kama watukutu, wakati Jim Iyke lazima aonekane mtu mbaya sana huku Mercy Johnson akijifanya mshamba na mtu wa kijijini au mwanafunzi.

Filamu nyingine maprodyuza wameziweka mpaka sehemu ya sita, lakini kitu hicho kingekuwa Hollywood kinaigizwa dakika zisizozidi 20 tu.

Mlinzi wa getini anafikia hatua ya kuwadharau mabosi wake tena mbele yao bila hata kufukuzwa au kupewa onyo.

Kila kitu kwenye filamu nyingi kinafanywa na mtu mmoja kuanzia kusambaza, kutengeneza, kuandika, kucheza, mapambo na kila kitu muhimu.

Wawili wanakubaliana chumbani lakini bado wanajifunika kwenye blanketi kubwa na bado wanavurugana kama kwamba wanafanyia mambo yao hadharani.

Filamu nyingi zinapendwa na wanawake hasa walioolewa kwa vile zinabeba hisia zao. Kwa mfano Wanaume dhaifu, lawama za ndugu na hata sumu ambayo kawekewa mume anailamba mama mkwe. Kila mtu anavyochapwa kofi linalia kama bunduki.

Akianza kutoa filamu Funke Akindele lazima Fathia Balogun ataiga na Femi Adebayo atafuata na kumalizia na Mercy Aigbe na jina na ujumbe wao utakuwa ni huohuo na watatoa haraka sana kwa kufuatana.

Unamwona msanii anakumbuka yaliyotokea mwaka 1972...lakini nyuma yake kuna bango la chagua Goodluck Jonathan 2011.

1 comments:

Anonymous said...

asieee ni kweli kabisaa ukiisoma hii utagungua mambo mengi sana yanayokosewa katika utengenezaji wa filamu na kwa wanaotengeneza wakiyapitia hayaaa natumaini watarekebisha na kuboresha filamu zao that gud

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms