Tuesday, June 19, 2012

....NIMECHOKA KUBANIWA JAMANI.....


MSANII Chipukizi katika tasnia ya filamu na vichekesho katika Swahiliwood, Maria Charles, ameilalamikia kampuni ya Al Riyamy Production ya jijini Dar es Salaam akidai inawafanyisha kazi nyingi lakini inaingiza filamu chache sokoni.

Kwa sasa nimeamua kusimama na kutafuta sehemu nyingine kwa ajili ya kuigiza. Kufanya kazi kwao haina maana, mtu unaigiza filamu nyingi ambazo zinafungiwa ndani tu," alisema.

"Unajua nyingine zinaweza kuja kuingizwa sokoni zikiwa zimepitwa na wakati jambo ambalo linaweza kutushusha hadhi kisanii maana teknolojia kila siku inakua,alisema Maria.

Msanii huyo ambaye ameshiriki kuigiza zaidi ya komedi 30, aliongeza kuwa kazi zilizotoka ambazo yeye ameigiza hazifiki hata nane.

Msemaji wa kampuni hiyo, Abdallah Khalfan, alisema kuwa suala la muda wa kutoa kazi ni suala la kampuni kwani mara nyingi wasanii wanapomaliza kazi hulipwa fedha zao.
"Si rahisi kuingiza filamu sokoni bila kuangalia soko lipo vipi," alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms