Monday, June 18, 2012

..........MKE WA PRINCE WILLIAM AWA KIVUTIO KWA UTARATIBU WAKE MPYA......


MKE wa Prince William, Kate Middleton, tayari amejijengea jina kwa mtindo wake wa kurudia nguo na viatu katika muda mfupi.

Kubwa kuliko yote ni ile aliyoifanya katika siku nne za kuadhimisha miaka sitini ya uongozi wa Malkia Elizabeth, ambapo alirudia viatu ndani ya siku tatu.

Hivi majuzi amerudia nguo ambayo aliivaa takribani miezi miwili iliyopita, alichoongezea ni kikofia tu juu, lakini viatu vilikuwa vilevile alivyovirudia wakati wa sherehe, kwa maana hiyo amevivaa viatu hivyo mara tatu ndani ya wiki mbili.

Takribani wiki mbili zilizopita, Kate alirudia nguo na viatu alivyowahi kuvaa katika hafla moja na kuzivaa katika harusi ya binamu yake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms