Monday, June 25, 2012

......MCHUMBA WA MR. BLUE AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME.... MR. BLUE SASA KUITWA BABA.....


MR Blue ambaye ni miongoni mwa wasanii waliowahi kufanya vizuri kwenye Bongofleva, amepata mtoto wa kiume mwanzoni mwa wiki hii.

Blue amepata mtoto huyo baada ya mchumba wake aliyewahi kumtambulisha kwa jina la Wahida, kujifungua jijini Dar es salaam.

"Nimevuka hatua moja kwenda nyingine. Kwa sasa mimi si mvulana tena ila ni baba, naitwa Baba Sameer," alisema huku akitabasamu.

"Nimeamua kumpa mtoto wangu jina hili maana naona linamfaa, kwani ni jina langu la pili ambalo nimekuwa nikilitumia kwa muda mrefu, pia ni jina la baba yangu."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms