Friday, June 15, 2012

.....LOL, AREJEA KIMYA KIMYA.....


MSANII maarufu wa Nollywood, Uche Jombo, amerejea kimya kimya Nigeria baada ya kufanya harusi ya siri huko Puerto Rico.
Mume wa mwanadada huyo ametajwa kwa jina la Kenny Rodriguez. Walifunga ndoa hiyo mwezi uliopita.
Uche alionekana Uwanja wa Ndege wa Muritala Mohammed jijini Lagos akirejea wikiendi iliyopita na hata marafiki zake wa karibu wamethibitisha kuwa kila kitu kilikwenda sawa.
Ingawa msanii huyo alikuwa mgumu kuzungumzia suala hilo, lakini imeelezwa kuwa baada ya mwezi huu itafanyika sherehe rasmi nchini Nigeria na mastaa wenzie wataalikwa.
Hata hivyo hadi sasa hawajaambiwa lolote kuhuiana na hafla hiyo zaidi ya kusoma kwenye magazeti tu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms