Tuesday, June 12, 2012

......BRITNEY SPEARS BADO NI MGONJWA.....


AFYA ya mwanamuziki, Britney Spears, bado ni tete kwani hivi karibuni wakati wa kurekodi kipindi cha X Factor, alilazimika kutoka nje mara mbili baada ya kuzidiwa.

Pamoja na kusumbuliwa na matatizo ya akili, Britney ana ugonjwa wa kushindwa kuwa makini kwa muda mrefu (Attention Deficit Hyperactivity Disorder) na ndiyo uliomfanya atoke katika kipindi.

Inaelezwa kuwa ugonjwa huo unatibika, lakini yeye hawezi kutumia dawa hizo kwa sasa kwa kuwa ana dozi nyingine kubwa ya matatizo ya akili.

Madaktari wamemshauri autibie ugonjwa huo kwa vyakula na ushauri wa wataalamu. Hata alipotoka nje ya kipindi, wataalamu hao walifika kumsaidia ili aweze kurudia katika hali yake.

Mmiliki wa shindano hilo, Simon Cowell, amemwekea Britney utaratibu wa kutoka nje wakati wa mapumziko ili aweze kufanya kazi hiyo vizuri.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms