Monday, May 28, 2012

........WILL SMITH AZUNGUMZIA KELBU....

MWIGIZAJI, Will Smith, kwa mara ya kwanza amezungumzia sababu za kumpiga kibao Mwandishi wa Habari wa kiume aliyetaka kumbusu.

Smith anasema ulikuwa wakati mgumu kwake na hakujua alipata wapi nguvu ya kumrushia kibao mwandishi huyo, kwani hakumbuki mara ya mwisho aliporusha ngumi ilikuwa lini.

"Mwandishi yule alinijia na kuniomba nimkumbatie kwa kuwa ni shabiki mkubwa wa kazi zangu, ghafla niliona nimebanwa na mtu analeta uso wake kwangu na kunibusu, nilijikuta tu nimempiga kibao," alisema Smith.

Hata hivyo mwandishi huyo wa Ukraine amemwomba msamaha Smith akikiri kuwa alivuka mipaka kwa kumbusu mwanaume mwenzake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms