Wednesday, May 2, 2012

........SIPENDI MAVAZI YANGU KUHUSISHWA NA ULOKOLE WANGU - DOKI.....

MSANII Ummy Wenceslaus, maarufu kama Dokii, ambaye awali alikuwa akiigiza kwa lafudhi ya Kikenya, amesema kuwa anashangazwa na watu ambao wamekuwa wakimsema au kumsengenya na kuwa na mashaka na wokovu wake.

Anasema kuwa ulokole wake hauingiliani na mavazi au staili ya nywele alivyonyoa na kuzisuka.

Watu wana maneno sana, kila Dokii akifanya kitu lazima waongee, wengine wanasema kwa nini Dokii akicheza anakata viuno sana wakati anajifanya mlokole? Mbona kanyoa vile!

"Binafsi najiamini kama nimeokoka na kukata viuno ni utamaduni tu, kama msanii naweza kufanya jambo lolote kwa ajili ya kuelimisha na kuburudisha na hakuna cha ziada, anasema Dokii.

Dokii anasema kuwa hajawahi kumkosoa Mungu kwa kujichubua ngozi yake kama walivyo baadhi ya waumini ambao pia nao wameokoka na kuhubiri, lakini watu wanamsema yeye kuhusu kucheza muziki, kuimba na kukataa viuno.

Amesema anashanga watu kuingiwa na hisia za ajabu na akahoji ni sehemu gani katika Biblia imeandikwa mtu asiche muziki.

Mimi sijali ya watu bali ndani ya nafsi yangu ndiyo najua wokovu wangu, kama unavyoniona, nimekuja na staili mpya kabisa ambayo nimeibuni mwenyewe na kuipa jina la 'Hakunaga kata ngebe man', najua watatesema

1 comments:

George said...

Kama vile huwezi kumtenganisha mtu na matendo yake ndivyo usivyoweza kumtenganisha Mungu na utakatifu wake. Unajua usipate shida na kujitesa; Neno la Mungu linasema utakuwa mtakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Kama Yesu wako ancheza miziki ya dunia una haki ya kufanya hivyo, kama Yesu wako anakata viuno hivyo unavyofanya basi endelea, kama Yesu wako anavaa vinguo vifupi wewe vaa kwa sababu Yesu wako ndivyo alivyo. Lakini Yesu tunayemwamini ni mtakatifu hachanganywi na uchafu wala hawekwi kwenye mitandao ili apate watetezi bali anajitetea mwenyewe. Neno la Mungu linasema ni bora uchague moja kuwa baridi au moto usiwe uvuguvugu maana atakutapika. Dada yangu Dokii Mungu anakupenda bado chukua hatua ya kumpa Yesu maisha yako mazima. Huwezi kumpenda Mungu na huku unayapenda ya dunia. Nakushauri umpende Mungu ya dunia ni ya kitambo tu. Usione unaendelea kuishi na kufanya unayoyafanya na kuuliza ni nini ulichokosea. Hiyo ni neema tu ya Mungu na unajua ni ya muda, muda ukifika utapita. Je utapata nafasi ya kuutetea uovu mbele za Mungu? Si unawafahamu wengi waliokuwa maarufu na wengine ni marafiki zako na sasa hawako tena? Je wanayo nafasi ya kuuliza maswali hayo ambayo unauliza ambayo nina hakika hata wewe mwenyewe una majibu yake? Tengeneza mambo ya nyumba yako dada yangu maana Neno la Mungu linasema utakufa hakika; ndivyo Mungu alimwambia nabii Hezakia. Hujachelewa bado Yesu anakupenda.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms