Wednesday, May 16, 2012

.....MALUMBANO YA NINI JAMANI??......


THEA amesikitishwa na malumbano ya upinzani uliopo kati ya makundi mawili ambayo ni Bongo Movie Club na Shirikisho la Vyama vya Wasanii wa filamu Tanzania (TAFF) akisisitiza kuwa malumbano hayo hayajengi.

"Mimi nasema kuwa hawa viongozi wa TAFF hawako makini, binafsi sipo katika kundi lolote siyo Bongo Movie wala hiyo TAFF kwa sababu sioni faida yake zaidi ya kupotezeana muda tu," alisema.

"Kama kuna kundi ambalo lipo kwa ajili ya kucheza mpira kwa nini TAFF ihangaike nayo hapa ndiyo utaona kuwa hatuna viongozi."

Thea anasema kuwa kutokana na kuwepo kwa makundi kumezidi kurudisha nyuma harakati za wasanii kujitafutia maslahi huku jamii ikiwaona kama ni watu wasio makini.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms