Thursday, May 3, 2012

.........MAISHA YANGU YAMEZUNGUKWA NA MITIHANI MIGUMU.....

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Wastara Juma Stara yupo katika wakati mgumu sana kutokana na kuuguliwa na mumewe mwigizaji mwenzake Sajuki.

Stara anasema alikuwa akipata faraja kutoka kwa Sajuki alipopata ajali na kupoteza mguu wake mmoja, lakini mambo yamebadilika sasa Sajuki anapata faraja kutoka kwake.

Kinachofanya nitabasamu ni kwa sababu namwamini Mungu, lakini moyo wangu unavuja damu, naumia sana, jamii inaniona ni mtu wa kulialia.

"Maisha yangu nimepitia mitihani mingi, umri wangu ni mdogo lakini nimekomaa kama mtu mwenye umri wa miaka sitini, nikiona matukio nasikitika lakini najua mengi na nimepitia mengi sana, maisha yangu yametawaliwa na mitihani, anasema Stara.

Stara anasema kuwa, tangu mwezi Julai alipoanza kumuguza Sajuki ilibidi kusimama kufanya kazi.

Baada ya kugundua kuwa ni mjamzito, madaktari walimshauri muda mwingi apumzike, lakini ilikuwa ni vigumu kwani hakuwa na msaada wowote.

Anasema, pamoja na matatizo hayo, aliamua kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuomba msaada kwa ndugu wa karibu.

Mara nyingi najifanya mjinga tu, lakini nimepitia mengi katika maisha, filamu ninazoigiza ni sehemu ya maisha yangu kuhusu mitihani niliyopitia, naumia sana lakini bado namshukru Mungu kwa kila jambo Mungu ana makusudi na mimi.

"Siku hizi ni vigumu kumtegemea ndugu au jamaa, kila mtu ana mambo yake yanayomkabili, si rahisi kutoa msaada kwako.

Sasa Stara anatafuta zaidi ya Sh 25 milioni kwa ajili ya matibabu ya Sajuki ambaye anatumia dawa zinazouzwa Dola 1,000 kila wiki.
Sajuki pia anatakiwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi mwezi huu wa Mei.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms