Monday, May 7, 2012

......BOBBY BROWN AJISAFISHA.....


MUME wa zamani wa marehemu, Whitney Houston amejisafisha kuwa hausiki na mwanamuziki huyo kujiingiza katika kutumia dawa za kulevya.

Bobby Brown amesema hata yeye kabla hajakutana na Whitney hakuwa akitumia dawa za kulevya, alianza kutumia baada ya kumuoa mwanamke huyo.

"Si kweli. Sikuwahi kutumia dawa za kulevya kabla sijakutana na Whitney, nilikuwa navuta bangi na kunywa pombe basi, kifupi siye mimi niliyemfundisha Whitney," alisema Brown.

Brown anasema ni ngumu kuelezea mwanamke huyo aliingiaje katika utumiaji wa dawa hizo, lakini anachojua yeye ni kuwa alianza kutumia hata kabla ya kuwa maarufu.

Hata hivyo Brown anasema kwa miaka yote aliishi kwa upendo na mkewe hata pale walipokuwa 'mateja' waliishi kwa kupendana kuliko watu walivyokuwa wakiona kwa nje.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms