Thursday, April 5, 2012

.....VIPODOZI VYAMTOA JASHO AMAH........

MWIGIZAJI, Grace Amah, inadaiwa alikwenda Uingereza na alipokuwa huko aliingia kwenye duka moja linalomilikiwa na Mnigeria na kuchukua vipodozi akiahidi kuwa angempelekea pesa kabla hajarudi Nigeria.

Lakini inaelezwa kuwa, Amah aliondoka Uingereza bila kwenda kulipa deni na wala kumtaafu Mnigeria mwenzake huyo kuwa anaondoka.

Mnigeria mwenye duka aliitafuta namba ya Amah na kumpigia, mwigizaji huyu aliahidi kuwa angemtumia pesa hiyo baada ya kuiomba akaunti yake ya benki, lakini hakufanya hivyo.

Bahati nzuri mume wa yule mwenye duka kule London alipata safari ya kwenda Nigeria, naye mkewe alimpa namba ya Amah alimpigia simu, lakini badala ya kupata fedha aliambulia maneno ya kashfa kutoka kwa mwigizaji huyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms