Monday, April 23, 2012

......SASA HIVI SIBAHATISHI NAGONGA NGOMA ZA UKWELI.....


MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye alitamba na kibao cha 'Kifungo Huru', amesema katika suala la muziki habahatishi tofauti na wengi wanavyodai.

Kwa kuthibitisha hilo, msanii huyo, C-Sir Madini, ameamua kutoa wimbo mwingine alioutambulisha kwa jina la 'Nishike Mkono'.

Msanii huyo ambaye bado ni mwanafunzi, anasema wakati mwingine anakuwa kimya kwenye anga za muziki kutokana na kutingwa na masomo.

"Masomo ndiyo yanayonifanya nishindwe kutoka mara kwa mara kutokana na nguvu nyingi kuzielekeza huko," alisema.
Kuhusu wimbon huo mpya, alisema tayari picha zake za video zimeshachukuliwa na amemshirikisha Benjamin Busungu..

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms