Sunday, April 8, 2012

......POLISI WATHIBITISHA KUMKAMATA LULU.......


Habari za awali za kipolisi ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Charles Kenyela amezitoa kwa waandishi kwa njia ya simu na kusikika kupitia EATV zinasema kuwa kulikuwa na hali ya kutoelewana kati ya Steven Kanumba na Mpenzi wake na chanzo ni wivu wa kimapenzi.Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika pale walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi wake Marehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi.
Taarifa za awali kabisa ambazo hazikuwa rasmi zilidai kuwa Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi wake ambaye ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.
Taarifa hizo ambazo bado hazina uthibitisho rasmi zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na ndipo aliposikia mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka kumuuliza ndipo mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusukumana Kanumba alianguka na kugonga kichwa chini.
Lulu ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18 tangu kuzaliwa.
. Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa Tanzania bali hata nje ya nchi pia. Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona katika kuigiza na kuvaa uhusika mbalimbali tofauti na nyota wengine hivyo kuwavutia watu wa rika zote. Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 ya uhai akiwa ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.
Mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha masikitiko yao ambapo kufika saa tisa usiku habari zilikuwa zikisambaa kama moto nyikani kupitia Facebook, Twitter na Blogs mbalimbali.Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika kwa taabu

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms