Sunday, April 29, 2012

.......NI KICHEKESHO NDANI YA JUKWAA......

NI kichekesho. Rapa Drake aliwashangaza mashabiki wake pale alipoanguka wakati akitumbuiza jukwaani huko Uingereza.

Kilichowachekesha mashabiki siyo kuanguka kwake, bali ni ujumbe aliokuwa akiutoa na kitendo hicho.

Inadaiwa rapa huyo alianguka wakati akiimba wimbo Take Care ambao tafsiri yake ni 'Kuwa mwangalifu'.

Kingine kilichowachekesha mashabiki ni kitendo cha rapa huyo kujifanya kama vile alipanga kuanguka na kujikusanya kistaili wakati wa kuinuka.

Walioharibu picha nzima ni mabaunsa ambao baada ya Drake kuanguka na wao kuona hawamuelewi elewi, walimfuata kumuangalia kama yuko sawa, naye alijikausha na kuendelea na onyesho.

Drake aliwahi kuanguka katika shoo mwaka 2009 wakati akiimba wimbo Best I Ever Had na kujitonesha goti lililokuwa likimsumbua.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms