Tuesday, April 3, 2012

...NATEGEMEA KUTEMBELEA WATOTO YATIMA NCHINI UGANDA........

MREMBO aliyewahi kuwa Miss Arusha mwaka 2008 ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo Grolia Emson ‘Kokoye’, amesema kuwa, anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uganda, ambapo ataondoka nchini April 9 mwaka huu na huku atakuwa kwa muda wiki tatu hadi nne.

Akizungumza, msanii huyo alisema kuwa ziara hiyo pia itakuwa na mambo mengi kama kutembelea baadhi ya vituo vya watoto yatima wa nchini humo pamoja na kurekodi ngoma zake kadhaa na wasanii wa huko.

Alisema kuwa kwa sasa bado hajajui ni wasanii gani ambao atafanya nao kazi lakini anaamini baada ya kuwasili huko atajua ni akina nani kwani wapow engi ambao anafirilia wanaweza kufanya kazi pamoja.

“Natajia kwenda nchini Uganda, na safari yangu itakuwa na mambo, na naweza kuondoka nchini tarehe za mwanzoni tu wa mwezi huu wa April na naomba watanzania wajue kwamba naenda kwa ajili ya kazi za muziki wa zangu mwenyewe binafsi,” alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms