Monday, April 23, 2012

....MZIMU WA KANUMBA WAANZA KUWATESA WASANII.........

KAMA kuna mtu anayeteseka baada ya kifo cha mwigizaji Steven Kanumba, basi ni mtoto Othman Njaidi OJ aliyeigiza naye kwenye filamu ya Uncle JJ.

OJ ambaye aliibuliwa kipaji chake na Kanumba, ameigiza pia filamu kadhaa zilizotamba.
Uchunguzi umebaini kuwa, tangu Kanumba afariki, mtoto huyo amekuwa mpweke na na hana raha huku staili yake ya maisha ikiwa imebadilika kwa kiasi kikubwa.
Ingawa mtoto huyo amekuwa hawezi kujieleza hali inayomkumba kutokana na upweke huo, habari zilizothibitishwa na wanafamilia zinasema kuwa hata kula analazimishwa na muda mwingi ni lazima asimamiwe na mama yake, jambo ambalo halikuwepo awali.

Hali hiyo imeenda mbali zaidi kwani baada ya mazishi ya Kanumba, OJ amekuwa akikurupuka usingizini na kupiga kelele akidai kutokewa na msanii huyo, jambo ambalo limemfanya mama yake kumchukua na kulala naye.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mama wa Othman, Hidaya Njaidi, alisema: "Mwanangu anapata shida sana tangu Kanumba afariki, usiku anashtuka na kupiga kelele, ukimuuliza nini anakwambia ni Kanumba kamtokea.

"Mara nyingi hali hii inamsumbua sana, ndiyo maana sasa nimeamua asilale peke yake. Nimemchukua nalala naye, kidogo naona hali hiyo inaanza kupungua.

"Ukiangalia hata uwezo wake wa kula umepungua, amekuwa mnyonge sana. Kila kitu inabidi kumsimamia, usipofanya hivyo anaweza asile kabisa, kwa hiyo nafanya kazi ya ziada kuhakikisha anarudi kwenye hali ya kawaida na kusahau yaliyopita.

"Alikuwa anafanya mambo mengi na Kanumba, ndiyo maana amekuwa hivi, walishazoweana na mara kwa mara alikuwa anakutana naye."

Alisema pia kuwa, mtoto huyo amekuwa na msongo wa mawazo na kila mara amekuwa akiuliza hatma yake kwenye fani ya uigizaji kwani anaona kama ndiyo mwisho wake.

Mama huyo anasema mtoto wake alikuwa na ndoto ya kuwa msanii mkubwa nchini na duniani miaka ijayo, lakini anahisi kama ndoto hiyo itafutika.

Kila siku anauliza swali moja tu kuwa 'mama kweli mimi nitaigiza tena kama nilivyokuwa na Anko Kanumba?
"Ninatumia muda mwingi kumbembeleza maana nahisi hali hiyo ikiendelea masomo yatamshinda, yupo katika majonzi mazito, aliongeza mama huyo ambaye anaishi na mwanaye Kimara Kona, Dar es Salaam.

Mama Njaidi anaelezea kuwa, mwanaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa Kanumba hata mikataba ya OJ ilisimamiwa na marehemu na kabla ya kifo alikuwa asimamie mkataba wa kazi ya mtoto huyo na kampuni moja ya Dar es Salaam.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms