Thursday, April 5, 2012

.....MATUMIZI YA UWOYA YANATISHA.....

WAKATI Watanzania wengi wanalalamikia ugumu wa maisha, hali ni tofauti kwa gwiji la filamu za Swahiliwood, Irene Uwoya, kwani yeye bajeti yake kwa siku ni zaidi ya mshahara wa mwezi wa watu wengi.

Habari zinasema kuwa katika suala la usafiri tu amekuwa akitumia gari la kifahari la kukodi, Range Rover, anayolipia Sh 450,000 kwa siku.

Mwanadada huyu ambaye mara nyingi filamu zake ni moja kati ya filamu ambazo hufanya vizuri sokoni, anaishi Kijitonyama katika moja ya nyumba yenye aliyopanga baada ya kuondoka kwao Mbezi.

Inasemekana kuwa Irene hapendi kutumia aina ya gari ambayo hata wasanii wengine wanaweza kutumia.

Lakini sasa imeelezwa ameachana na Range hiyo na amekodi Hammer ambayo kila baada ya siku nne anailipia Sh 4 milioni.

Mwandishi wetu aliongea na mmiliki wa magari hayo na kuthibitisha kulipwa fedha hizo na Uwoya. Hata hivyo mmiliki huyo hakupenda kutajwa jina gazetin

1 comments:

Anonymous said...

Aache kutudanganya, ingekuwa kweli si angejenga nyumba akae kwake? Mbona kapanga? Apeleke utumbo huko mfyuuuu...,

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms