Wednesday, April 18, 2012

......KWENYE UPANDE WA VIATU MIMI NATISHA ETI..........

RITA Dominic amesema yeye ni mkali inapokuja kwenye suala la viatu, lakini katika mavazi na fasheni zingine za urembo hatishi kama mastaa wengine.

Lakini anashangaa kwamba mashabiki wengi wanamsifu kwamba yuko juu kwenye uchaguzi wa mambo hayo wakati yeye anajiona kawaida sana.

"Sijioni kama mtu wa fasheni sana, mimi ni mkali kwenye ishu za viatu tu, lakini huko kwingine ni wa kawaida sana kama msichana mwingine yoyote yule.

"Nasema hivyo kwa vile najijua, sioni kitu kipya nilichonacho kuwazidi wenzangu. Napenda sana kuchanganyika na watu na kuwa makini sana inapokuja kwenye suala la kazi. Ninajijua kwamba nina jazba sana lakini najaribu kujituliza na kujishusha inapofika kwenye hiyo hali."

"Rita ni mtu mwenye huruma sana na msikivu, napenda sana kukaa nyumbani saa 24 kwa vile ukishakuwa staa kwenda mitaani ni tatizo, nakuwa sina uhuru kabisa."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms