Wednesday, March 21, 2012

........WAGHANA WAMFAGILIA KANUMBA.........

TAMASHA la filamu linalojulikana kama FOFA ambalo hufanyika kila mwaka Accra, Ghana lilitoa mwaliko kwa gwiji katika tasnia ya filamu Swahiliwood Steven Kanumba The Great kwenda nchini humo kupitisha filamu zitakazoonyeshwa katika tamasha hilo.

Kanumba kafanikiwa kuingiza filamu ya Devil's Kingdom.

Nilikuwa Ghana, nashukuru sana kwa mapokezi niliyopata kwa waandaaji wa tamasha hilo na kufanikiwa kuingiza filamu yangu ya Devil's Kingdom na kuweza kushinda baada ya filamu nyingi tu kushindwa kuchaguliwa kwa ajili ya tamasha hilo ambalo hushirikisha filamu nyingi kutoka Afrika, nimejifunza mambo mengi sana, alisema.

Filamu ya Devil's Kingdom imechaguliwa kama filamu yenye sauti bora, na Kanumba anasema kuwa amerudi kutoka Ghana, wapenzi wa kazi zake wajiandae kupokea zawadi ya filamu bora baada ya kukutana na watayarishaji mahiri ulimwenguni na kubadilishana mawazo.

Anasema ushindi wa filamu ya Devil's Kingdom ni mwanzo mzuri kuelekea katika ubora wa kimataifa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms