Wednesday, March 7, 2012

.....USANII NI KAZI NGUMU SANA......

Swahiliwood, Yuster Nyakachara Monica, amekiri kuwa kazi ya uigizaji ni ngumu hasa kama mhusika haungwi mkono na familia yake.

Na hili huwa tatizo kubwa kwa wanawake walio katika ndoa, ni ngumu kufanikiwa, alisema.

Sisi wasanii tunakabiriwa na changamoto kubwa tunapokuwa katika kurekodi filamu, hasa pale inapotokea kazi za usiku mara nyingi kama umeolewa mumeo kama si mwelewa, hawezi kukuruhusu.

Kwa mantiki hiyo lazima familia yako ikuunge mkono na kukubaliana na hayo, vinginevyo usanii utakushinda.

Monica ameolewa na ana watoto wawili na anamshukru Mungu akisema mume wake ni mwelewa na ana muunga mkono katika kazi yake.

Huwa nafikiria kama mume wangu asingekuwa mwelewa, halafu ndiyo natakiwa kwenda kurekodi usiku na fedha za watu nishalipwa, nisingeweza.

Msanii huyo ameigiza filamu kama Wekundu Wa Kuzimu, Subiani na Why This?

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms