Wednesday, March 14, 2012

......NIMEOKOKA KWA MAANA YA KUPATA WOKOVU......

MWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu na maigizo Swahiliwood, Julieth Samson Kemmy, kwa sasa maisha yake ameyakabidhi kwa Bwana baada ya kuokoka.

Sasa kila anapokuwapo anatamani kuwahubiria Injili wasanii wenzake na jamii inayomzunguka.

Kwa sasa msanii huyo anaonyesha kwa vitendo katika kumtangaza Masia, lakini anaamini kuokoka hakupingani na kazi yake ya uigizaji.

Hii ni kazi ambayo kama inatumika vizuri inaweza kusaidia jamii katika kubadilika na kutenda mema, si kila filamu lazima iwe na upotoshaji, alisema Kemmy.

Lakini pia ninaangalia uhusika wangu katika filamu, siwezi kuigiza filamu ambayo inapingana na neno la Mungu au hata kuigiza nikiwa na nguo ambazo hazikubaliki kijamii.

Kemmy ni moja kati ya wasanii waliolijenga kundi la Kaole Sanaa kwa uigizaji na utunzi wa maigizo yaliyoteka watazamaji wa televisheni.

Hivi karibuni ametunga filamu inayoitwa Diana ambayo anaamini kuwa ni filamu yenye ujumbe katika jamii.

2 comments:

Anonymous said...

hii kitu

Anonymous said...

Nakupa BIG UP ndugu yangu Kemmy kwa uamuzi wa kuokoka. Nadhani ni uamuzi mzuri sana. Wokovu ni kitu cha mhimu na wasnii wengine ni vizuri wakaiga mfano wako...

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms