Wednesday, March 14, 2012

..........NATAMANI KUZAA KWA SASA......

BINTI mrembo, Ini Edo, amekiri kwamba muda si mrefu na yeye atakuwa na mtoto na wala haogopi kupoteza shepu yake kutokana na uzazi.

Msanii huyo anasema kupoteza shepu ni kitu cha kawaida kwa vile lazima awe na mtoto hata kama ni miaka mingi ijayo.

Ninahitaji mtoto na nitampata punde, wala siogopi kwamba shepu yangu itaharibika. Lazima na mimi niwe na watoto, anasisitiza.

Ini pia anasema wala hajawahi kuwa na tabia ya kuvuta sigara katika maisha yake ya kawaida, bali anasema huwa anafanya hivyo tu kwenye uigizaji filamu.

Nilivuta sigara lini? Au kwa vile unaniona navuta kwenye runinga, mimi huwa sivuti, alisisitiza msanii huyo ambaye ni miongoni mwa mabinti wanaofanya vizuri kwenye tasnia hiyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms