Monday, March 12, 2012

........NAFIKIRIA KUACHANA NA SANAA MAZIMA.,....

MSANII wa filamu bongo Rehema Fabian, baada ya kutaka kunywa sumu kwa lengo la kujiua, sasa amefunguka na kudai kuwa anafikilia kujitoa kwenye kila kitu kinachohusiana na sanaa kwani anahitaji kufanya ishu zake mwenyewe.

Fabian alifunguka  na kueleza ishu hiyo kwani anaamini ndiyo iliyosababisha hadi kufikia hatua ya kutaka kutoa uhai wake.

Alisema kuwa hata hivyo bado anafikilia juu ya ishu hiyo kwani ni hatua ambayo anahitaji kumshiriki mtu ili aweze kumpa ushauri pamoja kuchangua kazi nyingine anayoweza kufanya.

“Nafikilia kuachana na mambo yote yanayohusu sanaa kwa sababu nashindwa kufanya mambo yangu ya maana kwa kuogopa watu hivyo naweza kujihusisha na biashara zangu mwenyewe,” alisema.

Mwandishi wa habari hizi alimuuliza swali msanii huyo, kwamba endapo ataamua kufanya biashara pekee anatafanya ishu gani ambayo itajenga maisha yake alijibu “Zipo biashara nyingi hata saluni naweza kufanya kwa sababu kazi ni kazi hivyo yoyote naweza fanya,”

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms