Monday, March 26, 2012

.......MZIMU WA RIHANNA WAWAGEUKIA WABUNIFU.......

MWANAMUZIKI, Rihanna, naye ameanza kufuata nyayo za Beyonce, Victoria Beckham, Diddy, Jay Z na wengine kwa kujiingiza katika ubunifu wa mavazi.

Pamoja na kuwa ameshabuni mitindo kadhaa, amesema ni mapema mno kuzionyesha kazi zake kwani anahitaji kupata heshima katika katika tasnia hiyo pia.
Rihanna amesema tayari kuna kazi ambazo amezitengeneza, lakini hawezi kuzitoa hivi hivi bila kupata ushauri wa watu anaowaamini ambao ni wabunifu wakubwa.
"Nimewaomba wabunifu wakubwa waziangalie kazi zangu kwanza, baadhi nimeshakutana nao lakini pia nitasubiri mpaka wote wazikague kwanza," alisema.
"Zipo ambazo zitabadilishwa kutokana ushauri, nyingine nitaziondoa kabisa kwa kuwa zipo ambazo tayari nimeambiwa hazifai, zitakazokubalika ndiyo zitakazoingizwa sokoni, nataka kila atakayenunua kazi yangu akubali kuwa niliumiza kichwa."

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms