Wednesday, March 21, 2012

......MASTAA WA SOKA WANAOONGOZA KWA KULIPWA MISHAHARA MIKUBWA, NA MALI ZAO.......


Moja kati ya nyumba anazomiliki Lionel Messi iliyoko Barcelona, stori kwa mujibu wa barcainfo.
 
Kwa mara nyingine tena Lionel Messi anatengeza kichwa cha habari baada ya kutwajwa kuwa mwanasoka anayelipwa mkwanja mrefu kuliko wote duniani, huku David Beckham akishika nafasi ya pili na Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya tatu.

Kutokana na ripoti iliyotolewa na jarida la France Football ambayo imetoka leo, mshambuliaji huyo wa Barcelona anaingiza Pound 33 million kwa mwaka kupitia mishahara na fedha za matangazo wakati LA Galaxy midfielder na mchezaji wa zamani wa Manchester United David Beckham ambaye amekuwa akiongoza kwa muda mrefu listi hii, amekuwa wa pili akiingiza pound milioni 31.5, wakati star wa Real Madrid Ronaldo akikusanya pound milioni 29.2 ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Samuel Eto’o nae yupo katika nafasi ya nne akiingiza pound milioni 23.3m huku Wayne Rooney akikamata nafasi ya tano na pound milioni 20.6.


..........Beckham ndani ya Rolls Royce....
.......Beckham akiwa mitaani Marekani na watoto wake, kwenye hii picha anaonekana kamkodolea macho yule mrembo pale pembeni....
 
Hii ni moja kati ya majumba ya kifahari ya Christiano Ronaldo anaeichezea Real Madrid.
Bwana Samuel Eto.
 
Wyne Rooney ndio muhusika wa hii kwa mujibu wa world football extra.
 
Bwana Wyne Rooney.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms