Wednesday, March 14, 2012

.....JAMANI TUSICHANGANYE KAZI NA MAPENZI.......

DAVINA amewataka watayarishaji wa filamu kuzingatia maadili na kuheshimu wasanii kwa kutochanganya kazi na mapenzi.

Anasema jambo hilo linawakumba zaidi wasanii wa kike wakati wa ufanyaji kazi, kwani wengi hudhalilishwa na baadhi ya watayarishaji.

Inanikera mno ninapoona mtayarishaji anatumia nafasi yake kuchukua wasanii wa kike kwa manufaa yao na si kwa ajili ya kazi, alisema Davina.

Ni vema watayarishaji wakaheshimu hisia zetu na kuamini kuwa tupo kwa ajili ya kufanya kazi na si mapenzi yasiyo na ridhaa.

Pia mwanadada huyu ambaye ni mkongwe katika tasnia hiyo ya filamu za Swahiliwood, anasikitishwa na baadhi ya wasanii wenzake ambao wameandamwa na kashfa kila kukicha na anawaomba wabadilike.

Hawa wenzetu wanatudhalilisha kwa kashfa zao, hivi sasa msanii wa kike unaona hata aibu kujitambulisha kuwa wewe ni mwigizaji, kwani jamii inatuona wote tuna tabia za ajabu, jamani tubadilike, anasisitiza.

1 comments:

Anonymous said...

Mnh wewe je? mimi nadhani kwa wale wanaotutia aibu hasa hapa kwenye club yetu ya Bongomovie, Davina anaongoza kwa maskendo, ukimwona kama vile mpole na kucheka cheka sana lkn heshima hana mwanamke huyu, hapo alipo anatia aibu, sisi ndo tunaona aibu kuwa naye,...

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms