Friday, February 3, 2012

.......VIDEO ZA NYIMBO ZANGU MBILI 'MAWAZO NA NIMPENDE NANI' ZITAKUWA BOMBA MBAYA - DIAMOND.......

MSANII wa muziki wa kizazi kipya ndani ya ardhi ya bongo Diamond, amesema  anatarajia kuzitoa video ya nyimbo zake mbili ambazo ni ‘Mawazo’ na ‘Nimpende Nani’,ambapo kwa sasa  yupo katika mchakato huo.

Msanii huyu, alisema kuwa nyimbo hizo ndizo zinazomfanya awe bize kwa sasa kwani anahitaji kuzitoa katika kiwango cha kimataifa.

Alisema kuwa zipo nyimbo nyingi ambazo anahitaji kuzifanyia video lakini kutokana na ubora wa kazi hizo, hana budi kufanya hivyo kwani anaamini tangu alipozitoa zimefanya vizuri sokoni kiasi cha kuteka mashabiki wengi.

Hata hivyo msanii huyo aliuzungumzia wimbo wake wa ‘Nimpende Nani’, kwamba aliutunga kwa ajili ya mashabiki wake na siyo kwa maalumu kwa Wema Sepetu na Jokate Mwegelo kama ilivyotafsiliwa na watu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms