Wednesday, February 22, 2012

.........VANITA KUNG'AA BOMBA ILE MBAYA.......

MWIGIZAJI na mpambaji wa wasanii Swahiliwood, Vanita Omary amejikuta akiwa mwenye muonekano mpya na tofauti baada ya uzazi wa mtoto wake wa kike anayeitwa Precious ambaye kwa sasa ana miezi kadhaa.

Vanita kwa wengi wanaomkumbuka alikuwa na mwili wa wastani, kichwani kwake akiwa na rasta kama Bob, lakini sasa amenenepa na kunyoa rasta zake na kuwa na muonekano mpya tofauti na awali kama wengi walivyozowea kumwona.

Nashukuru Mungu kwa kunijalia mtoto mzuri Precious na kunipa afya njema kama unavyoniona. Ujio wa mwanangu umekuwa wa baraka kwangu, nimenepa japo sasa inabidi kununua nguo nyingine maana nguo zangu za zamani hazinitoshi tena.

Nimekuwa mama kweli hata sehemu ambazo nikianza kuigiza zitabadilika na kuingia katika kundi la watu wenye afya zao, anaongea katika hali ya utani Vanita.

Msanii huyo ambaye ni mahiri katika upambaji wa wasanii (Make Up Arts) ameolewa na msanii mwenzake ambaye ni Poulinus Mtendah, ambaye ni muongozaji wa filamu na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Waongozaji wa Filamu Swahiliwood.

Wote kwa pamoja wanafurahia ujio wa mtoto wao Precious.
Vanita alijizolea umaarufu katika igizo lililowahi kutikisa siku za nyuma katika televisheni ya TBC 1 la Jumba la Dhahabu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms